Na Mwandishi Wetu
Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Kigoma(DCC) imependekeza na kupitisha azimio la kugawa Kata (05) na upatikanaji wa Jimbo la Ujiji kwa lengo la kusogeza huduma karibu na Wananchi.
Maazimio hayo yamejadiliwa Leo March 13, 2025 katika kikao kilichoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr. Rashid Chuachua.
Katika kikao hicho Wajumbe wamejadili na kupendekeza kugawa Kata ya Kibirizi na kupata Kata ya Butunga, Kata ya Gungu na kupata Kata ya Gezaulole na Masanga, Kata ya Buzebazeba na kupata Kata ya Burega, Kata ya Mwanga Kusini kupata Kata ya Kilimahewa, Kata ya Mwanga Kaskazini kupata Kata ya Nazareti.
Aidha Wajumbe wa Kikao hicho wamejadili na kuazimia upatikanaji wa Jimbo la Ujiji kutoka katika Jimbo la Kigoma Mjini.
Akifunga kikao hicho Mkuu wa Wilaya amesema mapendekezo ya maazimio hayo yanatarajiwa kuwasilishwa katika Kikao cha Maendeleo ya Mkoa (RCC) ili kuendelea na hatua zaidi katika upatikanaji wa maeneo hayo ya Utawala.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa