Na Mwandishi Wetu
Waratibu elimu Kata na Walimu Wakuu wa Shule za Awali na Msingi Kata ya Mwanga kaskazini na Kusini Manispaa ya Kigoma/Ujiji wamepata mafunzo ya kuwawezesha kubainisha Wanafunzi wenye mahitaji maalumu.
Mafunzo hayo yamefanyika Leo June 23, 2025 katika Shule ya Msingi Uhuru yakitolewa na Timu ya ubainishaji wa Wanafunzi wenye mahitaji maalumu ngazi ya Halmashauri
chini ya Mradi wa Shule bora unafadhiliwa na Serikali ya Uingereza Kupitia Mfuko wa UK aid.
Akifungua mafunzo hayo Afisa elimu maalumu Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Ezekiel Mpanda amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia ubainishaji huo kwa lengo la kuboresha suala la ufundishaji na ujifunzaji kwa usawa.
Wakibainisha Wanafunzi wenye mahitaji maalumu wamesema miongoni mwao ni pamoja na Yatima, Viziwi, Albino, wenye ulemavu wa viungo, Usonji, Changamoto za ujifunzaji, wenye Vipawa na vipaji.
Waratibu elimu Kata na Walimu Wakuu waliopata mafunzo hayo ni Kutoka Shule za Awali na Msingi ambazo ni Mwanga, Mwenge, Katubuka, Dr. Martin Luther,Muungano, Kilimahewa, Uhuru, na Shule ya Msingi Carmel.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa