Na Mwandishi Wetu
Vijana kutoka familia za wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Manispaa ya Kigoma/Ujiji ambao wamepata mafunzo ya fani mbalimbali wametakiwa kujiunga pamoja katika vikundi ili kupata sifa ya kupata mikopo ya 10% kutoka Manispaa
Elimu hiyo imetolewa Leo March 16, 2023 na Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Gungu Bi. Leah Ngunyale katika chuo cha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya ufundi Standi (VETA) cha Mkoani Kigoma
Mtaalamu huyo amewataka kujiunga na kufanya kazi kwa ushirikiano kwa kuunda na kuvisajiri vikundi ambapo wanachama wake watakuwa na sifa ya kukopeshwa katika mikopo isiyokuwa na riba inayotolewa na kila Halmashauri, vikundi vya vijana vikinufaika kwa asilimia nne (4%)
Taasisi ya Elimu Nchini Tanzania ikishirikiana na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya ufundi Standi (VETA) na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Wamewawezesha Vijana kutoka familia za Wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Manispaa ya Kigoma/Ujiji hamsini na tatu (53) ambapo kumi na tisa (19) tayari wamehitimu mafunzo na vijana thelathini na nne (34) wanaendelea katika fani za Upishi, Mapambo, Udereva, Computa , Ubunifu, Ushonaji na Teknolojia ya nguo
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa