Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba amewataka Maafisa Watendaji Kata kuendelea kusimamia vyanzo vya Mapato na usimamizi wa miradi ya Maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika maeneo yao.
Agizo hilo amelitoa Leo Novemba 14, 2025 alipofanya kikao na Watumishi hao kwa lengo la kujadili utendaji kazi na usimamizi wa Shughuli mbalimbali za maendeleo.
Amewataka kutembelea na kukagua miradi inayotekelezwa kila mara ili kuhakikisha kunakuwa na miundombinu bora na imara itakayonufaisha Jamii kwa kipindi cha mda mrefu na kuendelea kuhamasisha Wananchi kushiriki Usafi wa Mazingira katika maeneo yao.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa