Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Salum Hamis Kalli amezitaka familia za Manispaa ya Kigoma Ujiji kufanya vikao vya Kifamilia katika kutatua changamoto za kimaisha ili kuepuka vitendo vya ukatili.
Ameyasema hayo Leo Desemba 07, 2023 katika maadhimisho ya Siku kumi na sita (16) za kupinga vitendo vya ukatili kwa Wanawake na Watoto yaliyofanyika Kata ya Kibirizi Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Amesema ukimya katika familia kunaweza kupelekea vitendo vya ukatili hivyo ni mhimu familia kukaa pamoja katika kutatua matatizo kwa pamoja.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Mwantum Mgonja amewataka Wananchi kuhakikisha Watoto wanapatiwa haki ya elimu, kutoa taarifa za Vitendo vya ukatili katika Mamlaka zinazohusika na kuepuka ukatili wa Kiuchumi na ngono kwa Wanawake Wajasiriamali.
Maadhimisho yameandaliwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo wakishirikiana na Wadau mbalimbali wakiwemo BAKAIDS na Kauli Mbiu ya Mwaka huu ni, Wekeza: Kuzuia Ukatili wa Kijinsia.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa