Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba amesema huduma za afya na Matibabu zinapatikana Katika Kata zote za Manispaa ya Kigoma/Ujiji pasipo Mwananchi kutembea umbali mrefu.
Ameyasema hayo Leo Desemba 04, 2025 alipokuwa katika kipindi cha #Sikumpya kinachorushwa na Main FM iliyopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
"Katika Manispaa ambazo Mwananchi hawezi kutembelea umbali wa Km 3 kufuata huduma ya matibabu ni Manispaa ya Kigoma/Ujiji" Amesema Mkurugenzi huyo
Amesema Halmashauri hiyo imeendelea kujenga Zahanati na kuboresha vituo vya afya kupitia Mapato ya ndani huku akisema kwa sasa jitihada zinazofanyika ni za kuimarisha ubora wa huduma.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa