Na Mwandishi Wetu
Wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji wanatarajia kunufaika na upataji wa hati miliki za ardhi zaidi ya elfu kumi (10,000) bure katika Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki Ardhi (Land Tenure Improvement Project)
Yamesemwa hayo na mratibu wa Mradi Manispa ya Kigoma/Ujiji Ndugu.Steven Ambrose katika kipindi cha #SikuMpya kinachorushwa na Main FM 91.7 Kigoma
Amesema mradi huo unafadhiliwa na Benki ya Dunia (WB) kwa lengo la kurasimisha ardhi na upangaji mji ili kuwa na makazi Salama katika Kata tisa (09) za Kibirizi, kasingirima, Kagera, Gungu, Businde, Rubuga, Majengo, Kitongoni na Kasimbu
Amesema kwa Sasa tayari Wanawanchi wamehamasishwa na wamepata elimu kwa kufanya mikutano katika Kata zinazohusika ili kushiriki katika zoezi hilo
Afisa Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ndugu. Martin Mwitula amesema mradi unahusisha Halmashauri 41 na unatarajia kutekelezwa kwa mda wa miaka 5 hadi Mwaka 2027
Amesema maeneo ambayo ujenzi umejengwa kiholela Wananchi na wamiliki wa ardhi watatambuliwa na kupatiwa Leseni za Makazi
Katika mradi huo Hati Milki za Ardhi milioni moja zinatarajia kutolewa Nchini, Ujenzi na ukarabati wa ofisi za ardhi, Uboreshaji wa ofisi za Mabaraza ya Ardhi, ukarabati wa masijala za ardhi, na kuwajengea uwezo watumishi pamoja na uratibu wa masuala ya kijamii na mazingira
zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa