Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr Rashid ChuaChua ameendelea kusisitiza usimamizi wa upatikanaji wa chakula kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari na Msingi kwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Ameyasema hayo Leo Januari 22,2025 katika kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Shughuli za lishe kwa kipindi cha Julai- Septemba, na Oktoba- Disemba 2024/2025.
Kiongozi huyo amewataka Watendaji wa Kata Kushirikiana na Wazazi, Jamii na Kamati za Shule kuhakikisha suala la lishe kwa Wanafunzi linatekelezwa ili kuinua kiwango cha ufaulu na kuepuka udumavu.
Amewataka Maafisa elimu kusimamia kilimo cha bustani shuleni na kusisitiza kufanyika majiko darasa katika vipindi vya masomo ili Wanafunzi kujifunza uandaaji wa Chakula bora.
Awali akiwasilisha taarifa za utekelezaji wa afua za lishe, Afisa lishe Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Omary Kibwana amesema Shule za Msingi na Sekondari ishirini na tano (25) Kati ya Shule hamsini na tisa (59) sawa na 42.4% ndizo zinatoa Chakula kwa Wanafunzi.
Amesema kwa kipindi cha robo ya kwanza na ya pili jumla ya Mitaa sitini na nne (64) Kati ya sitini na nane (68) ilifanya maazimisho ya Siku ya afya na lishe ambapo watoto 39,702 walipimwa hali ya lishe Kati ya 44,703 waliotarajiwa huku kaya 9629 Kati ya kaya 16331 zenye Wajawazito na Watoto wa umri wa chini ya Miaka 5 zilitembelewa na Wahudumu wa afya ngazi ya jamii (CHWs) Sawa na 59% ya Walengwa.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa