Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Ester Alexander Mahawe amewataka Wakazi wa Wilaya ya Kigoma kuanzia umri wa miaka kumi na nane (18) na kuendelea kujitokeza kupata chanjo ya UVIKO-19 katika kampeni ya Kitaifa ya Nyumba kwa nyumba na vituo vya kutolea afya itakayofanyika kwa mda wa siku saba(07)
Ameyasema hayo alipohutubia Wajumbe wa Kikao cha cha Afya Msingi ngazi ya Wilaya kilichofanyikia Leo Oktoba12, katika Ukumbi wa Redcross Kikihusisha Kamati ya Ulinzi na Usalama, Wakuu wa Idara na Vitengo, Waratibu wa Afya, kamati za afya za Wilaya, Viongozi wa dini, na Wazee Maarufu
Mkuu huyo wa Wilaya amesema utoaji wa chanjo ya UVIKO -19 unatarajia kuanza Oktoba 17-24 mwaka huu huku zaidi ya asilimia themanini (80%) ya Wakazi wa Wilaya ya Kigoma tayari wamepata chanjo ya Kujikinga na Ugonjwa wa Uviko-19
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amewataka Wataalamu wa Afya kuendelea kutoa elimu kupitia Matangazo ya sauti, picha na Vyombo vya habari ili Wananchi Kushiriki kikamilifu na kuendelea kuchukua tahadhari za Kujikinga na UVIKO-19
Amewataka Viongozi wa Dini na Wazee Maarufu kuendelea kuelimisha jamii namna ambavyo mtu aliyechanja anakuwa na nafasi kubwa ya kutoambukizwa ugonjwa huo na kuwataka kuendelea kuelimisha jamii kuepukana na dhana potofu
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Dr. Hashimu Mvogogo amesema zaidi ya Watu elfu arobaini na saba ( 47, 717) wa Wilaya ya Kigoma wanatarajia kuchanja Sawa na 20% ambao hawajachanjwa huku Watu 23, 157 wakiwa wa kazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji na Watu zaidi ya elfu ishirini na tatu ( 23, 157) wakiwa wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma
Ameendelea kusema zoezi hili litafanyika ambapo wahudumu wa Afya watapita nyumba kwa nyumba na katika Maeneo ya biashara huku chanjo zingine zikipatikana katika vituo vya afya
Chanjo ya UVIKO-19 itatolewa kwa ambao bado hawajachanja na Chanjo zitakazotolewa ni chanjo ya Jassen, Sinopharm, na Sonovac, ambapo tayari timu ya Watu sabini na nne (74) Manispaa ya Kigoma/Ujiji za Wachanji , Wahamasishaji na Watakwimu tayari wamepata mafunzo namna ya utoaji huduma
Zaidi endelea kutembelea www.kigomaujijimc.go.tz pamoja na mitandao yake ya kijamii
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa