Na Mwandishi Wetu
Kamati ya fedha na Uongozi Manispaa ya Kigoma/Ujiji Leo Novemba 23, 2022 imefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Kata mbalimbali za Manispaa hiyo
Ziara hiyo imefanyika ikiongozwa na Naibu Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Mgeni Kakolwa ambapo miradi mbalimbali ya Elimu, Afya , Kilimo na Biashara imetembelewa huku Viongozi hao wakitoa maagizo katika miradi ambayo haijakamilika
Katika ziara hiyo miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa Zahanati mpya ya Kibirizi, Ujenzi wa Zahanati ya Machinjioni kwa Mapato ya ndani, Ujenzi wa jengo la Wagonjwa wa nje ( OPD), Maabara na jengo la kufuria mavazi katika kituo cha afya cha Gungu kinachojengwa kwa gharama ya Tsh 300, 000, 000/= ikiwa ni fedha kutoka Serikali Kuu
Miradi mingine iliyotembelewa ni pamoja na Ujenzi wa vyumba vya madarasa kumi na Moja (11) katika Shule ya Sekondari Gungu kwa gharama ya fedha za Kitanzania Million mia mbili ishirini ( Tsh 220, 000, 000/=) , Ujenzi wa Kituo cha afya cha Buhanda kwa gharama ya fedha za Kitanzania Million (Tsh 500, 000, 000/=) ambapo Kituo hicho kimeanza kutumika,
Aidha mradi Kitalu cha Miche ya michikichi ya Kisasa aina ya Tenera umetembelewa ambapo kwa sasa imezalisha miche zaidi ya elfu ishirini na nne (24628) na inatarajiwa kugawiwa kwa Wakulima sabini na sita (76) ambao tayari wamewasilisha Maombi yao na mashamba ya wakulima thelathini na sita tayari yamekaguliwa (36) kwa ajili ya kugawiwa miche hiyo ya kisasa
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa