Katibu wa serikali za mitaa Mkoa wa Kigoma Ndugu. Moses Musuluzya amewataka wadau mbalimbali kuungana kwa ajili ya kupinga vitendo vya ukatii vya wanawake na watoto .
Ameyasema leo may 3, katika ukumbi wa halmashauri ya manispaa ya Kigoma/Ujiji katika kikao kilichohusisha halmashauri mbili, halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/ujiji na halmashauri ya Kigoma vijijini.
Katika kikao hicho ambacho lengo lake ni viongozi wa mkoa kufatilia utekelezaji wa namna ya kupinga ukatili wa watoto na wanawake ulivyotekelezeka katika halmashauri zote mbili kwa kipindi cha julai 2018 hadi march 2019 ikiwa ni ziara inayofanyika mkoa mzima wa Kigoma.
Akiwasilisha taarifa katika kikao hicho Afisa Ustawi wa jamii manispaa ya Kigoma/Ujiji bi. Agnes Punjira amesema halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji imefanikiwa kuwapata watoto 51 wanaoishi mtaani na katika mazingira magumu na kuwaunganisha na wazazi wao 19 na wazazi hao kufunguliwa mashtaka ili wapelekwe mahakamani kwa kosa la kutelekeza watoto.
Aidha ameendelea kusema MTAKUWWA Manispaa ya Kigoma/Ujiji imeendelea kuzijengea kamati 5 za kata ambapo jumla ya washiriki 90 tayari wameshapata mafunzo ya namna ya kupinga ukatili wa wanawake na watoto na mashauri 171 tayari yameshapelekwa mahakamani na kusikilizwa , na mashauri 97 yameshapatiwa ufumbuzi na mashauri 74 yalipatiwa rufaa.
Ameendelea kusema jumla ya kiasi cha Shilingi 5,001,500/= zimekusanywa kwa ajili ya matunzo kwa watoto walio katika ndoa zenye migogoro na waliozaliwa nje ya ndoa kwa kipindi cha julai 2018 hadi machi 2019
Ameendelea kusema kesi nyingi wanazokutana nazo katika utendaji kazi ni pamoja na ulawiti, kutia mimba, kubaka na kutelekeza familia ya mke na watoto
Ameendelea kusema licha ya mafanikio waliyoyapata zipo changamoto zinazoendelea kuwakabili ikiwa ni pamoja na uhaba wa bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za kupinga ukatili wa wanawake na watoto pamoja na uchache wa maafisa ustawi wa jamii .
Naye Afisa wa jeshi la Polisi (OCD) wa mkoa wa Kigoma Ndugu. Mayunga R. Mayunga akitoa taarifa katika kikao hicho amesema jeshi la polisi linafanya kazi katika kuhakikisha vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto vinapotea na tayari katika mitaa kuna polisi jamii lakini pia lipo dawati la jinsia linaloshughulikia vitendo vya uharifu kama vile vitisho vya maneno na vitendo.
Ameendelea kusema licha ya mafanikio ya kesi kufikishwa mahakamani ipo ya changamoto ya mashahidi wa kesi hizo kutofika kwa wakati na wengine kutokuwa tayari kutoa ushahidi kwa vitendo hivyo vya ukatili vinavyofanyika kutokana na vitisho vya familia au jamii.
Naye mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Mwailwa Smith Pangani amesema ofsi ya ustawi wa jamii itaendelea kuwekewa mazingira mazuri ya kutekeleza majukumu yao kwa kuwapatia ofsi yenye vigezo vya utekelezaji wa majukumu ya kupinga ukatili kwa wanawake na watoto.
Ameendelea kusema licha ya bajeti iliyopita kutotengwa kwa bajeti ya utekelezaji wa shughuli za MTAKUWWA katika marekebisho na utekelezaji wa bajeti mpya mwezi jan 2020 atahakikisha kiasi cha fedha kimetengwa kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao.
Naye katibu Tawala serikali za mitaa Mkoa wa Kigoma Ndugu. Moses Msuluzya amesema wapo watu wanaofadhili makundi ya watoto wanaoishi mtaani kwa lengo la kufanya uharifu jambo hilo halikubaliki na kuwataka vyombo vinavyohusika kuwachukulia hatua zina zofaa na kuendelea kusema wapo watu pia katika jamii wanaozuia jitihada za maafisa ustawi wa jamii na jeshi la polisi katika kutekeleza majukumu yao kwamba ni lazima wachukuliwe hatua kali.
Amehitimisha kwa kusema zipo changamoto nyingi katika kutekeleza majukumu hayo juhudi na nguvu nyingi zinahitajika kwa kuhakikisha wananchi, watendaji wa kata na mitaa, ustawi wa jamii, jeshi la polisi, mahakama na mashirika ya serikali na binafsi yana ungana kwa kuhakikisha vitendo hivyo vya ukatili vinapungua na kupotea kabisa.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa