Hali ya chakula halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/ujiji imeonekana kuzidi mahitaji ya wakazi hali inayofanya kuwa na chakula cha ziada katika manispaa hiyo.
Hayo yalibainishwa july 19, katika kikao cha kamati ya lishe wilaya kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji kikiwa na lengo la kuboresha hali ya ulaji wa vyakula bora kwa wakazi wa manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Katika kikao hicho kilichoratibiwa chini ya idara ya Afya kikifadhiliwa na IMA-World Hearth kikihusisha Mkurugenzi wa manispaa, wataalamu wa Manispaa , madaktari, viongozi wa dini na waandishi wa habari ambapo ilibainika kuwa na chakula cha kutosha na kuzidi kulingana na idadi ya wakazi.
Akiwasilisha katika kikao hicho Kaimu Mkuu wa idara ya Kilimo Ndugu. Jackson Kahabi alisema kwa sasa halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji ina chakula cha kutosha na cha ziada hali ambayo wakazi wa manispaa hiyo wanapaswa kukitumia kwa usahihi katika ulaji wao ili kuboresha afya zao.
Aliendelea kusema kwa sasa chakula cha wanga kilichopo katika manispaa hiyo ni Tani 85,850 ambapo mahitaji ya wakazi wa manispaa hiyo ikiwa ni Tani 61,238.3, ziada ya chakula cha Wanga ikiwa ni Tani 24,611.7 na chakula cha Protini ikiwa na Tani 10,650 zilizopo, Huku akiendelea kukazia kwa mtu mzima ulaji wa chakula cha wanga kwa mwaka ni Tani 3, huku mtoto mdogo akitumia Tani 0.15 kwa mwaka.
Naye afisa Mifugo na Uvuvi wa manispaa Ndugu. Lisapita J Ndila akiwasilisha taarifa katika kikao hicho alisema kwa sasa wanaendelea kutoa elimu kwa wavuvi kuhusu athari zitokanazo na mazao ya uvuvi yanayovuliwa kwa sumu huku wakichukua hatua sitahiki kwa wale wanaokutwa wakifanya uvuaji huo halamu.
Aliendelea kutoa takwimu kwa Protini zingine zinazozalishwa ambapo ameeleza kwa kipindi cha robo mwaka Aprili hadi june kilogram 177,960 za mazao ya nyama ya N’gombe yamezalishwa, nyama ya mbuzi ikiwa ni kilogram 8,694, nyama ya kondoo kilogram ikiwa ni kilogram 468, nyama ya Nguruwe ikiwa ni kilogram 54,180, nyama ya kuku ikiwa ni kilogram 1,836, samaki ikiwa ni kilogram 51,240, dagaa zikiwa zimedhalishwa kilogram 4,257, maziwa yaliyozalishwa yakiwa lita 32,641 na mayai yaliyozalishwa yakiwa ni 454,892 ambapo uzalishaji huo ni wa wastani jambo linalofidiwa na Protini zingine zinazoingia kutoka katika halmashauri zingine.
Aliendelea kusema katika kuendelea kuboresha hali ya lishe katika Manispaa hiyo wameweza kutembelea wafugaji 459 na kutoa elimu ya namna wanavyopaswa kuzalisha na namna ya kuvuna mifugo hiyo na kanuni za lishe ili kuboresha afya zao na wafugaji 25 wa samaki wenye mabwawa 65 wakiwa wametembelewa na kupata elimu ya ulaji bora.
Naye Afisa lishe wa Manispaa hiyo Ndugu. Juma Nziajose alisema halmashauri imeendelea kutoa elimu kuhusu masuala ya lishe kwa kufanya ziara katika shule za msingi na sekondari na kutoa elimu kwa wanafunzi na walimu huku elimu pia ikifanyika katika vikundi vya kijamii vya wanawake na wanaume vilivyopo katika manispaa hiyo kupitia kwa maafisa maendeleo ya jamii.
Aliendelea kusema hali ya udumavu inaendelea kupungua katika manispaa hiyo licha ya kata ya Gungu kuongoza kwa udumavu katika manispaa hiyo hali inayofanya elimu ielekezwe kwa kina katika kata hiyo kwa kuwapatia elimu akina mama wajawazito na waliojifungua , wazazi wa kiume namna ya kuhudumia familia kuanzia mimba kutungwa hadi umri wa utu uzima.
Naye kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndugu. Emmanuel Katemi aliwataka wakuu wa idara, viongozi wa dini na waandishi wa habari kuendelea kutoa elimu ya lishe katika maeneo yao ya kazi na kuhakikisha ni jambo linalotiliwa mkazo ili kupata taifa lenye watu wachapa kazi kwa ukamilifu katika kufikia malengo ya halmashauri na Taifa kwa Ujumla.
Aliendelea kuwataka wakazi wa manispaa ya Kigoma/Ujiji kuendelea kutumia vyakula vilivyopo ikiwa manispaa hiyo ina vyakula vya kutosha na ziada kutokana na vyakula vingi vinavyoingia kutoka katika halmashauri zingine.
picha zaidi ingia katika maktaba ya picha www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa