Na Mwandishi Wetu
Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kigoma Leo Januari 17, 2022 imefanya ziara ya kutembelea utekelezaji wa Ilani Manispaa ya Kigoma/Ujiji huku wajumbe wakipongeza ubora wa ujenzi wa vyumba vya madarasa ambao umekamilika
Pongezi hizo zimetolewa na wajumbe wa kamati hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Ndugu. Amandus Nzamba mara baada ya kufanya ziara katika Shule ya Sekondari Buteko, Gungu, Buhanda na Shule ya Sekondari Kigoma/Ujiji
Mwenyekiti huyo amesema kamati imeridhishwa na ujenzi wa vyumba 48 vilivyojengwa kutokana na fedha za Ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko-19 huku akiwataka Madiwani wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kuendelea kusimamia Wataalamu katika miradi na kupata matokeo yenye ubora na kuwànufaisha wananchi walio wengi
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Ndugu. Thobias Andengenye akiongea na Wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao wameanza masomo yao katika madarasa hayo amewataka kusoma kwa bidii na kuhakikisha wanatumia na kutunza miundombinu ya madarasa, viti na Meza
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Frednand Filimbi awali akiwasilisha taarifa amesema Manispaa hiyo ilipokea kiasi cha Fedha Million Mia tisa sitini (Tsh 960,000,000/=) kutoka Serikali Kuu kwa lengo la ujenzi wa vyumba vya madarasa 48 kwa shule 16 na kusema Ujenzi huo umekamilika kwa wakati
Ameendelea kusema kukamilika kwa Ujenzi huo wa vyumba vya madarasa utawanufaisha mwanafunzi zaidi ya Elfu mbili mia nne (2400) na kukuza mazingira ya Ufundishaji na Ujifunzaji huku akisema tayari wanafunzi wameanza kuyatumia madarasa hayo
Miradi mingine iliyotembelewa na Kukaguliwa ni Ujenzi wa Chanzo cha Maji Amani Beach, Ujenzi wa Machinjio ya Ujiji yenye thamani ya Mradi Million Mia mbili hamsini (Tsh 250,000,000/=) hadi kukamilika, Ujenzi wa Zahanati ya Rusimbi, Ujenzi wa barabara za Legeza Mwendo yenye urefu wa Km 0.56 gharama ya Mradi ikiwa ni Tsh 509, 864,505.00/= , Barabara ya Mabatini yenye urefu wa Km 0.6, na Ujenzi wa barabara ya Muungano "B" kwa Kiwango cha lami tabaka mbili yenye urefu wa Km 0.22 zikijengwa kwa gharama ya Tsh 499,999,200.00/= ikiwa ni fedha zitokanazo na Tozo za Mafuta Nchini
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa