Na Mwandishi wetu
Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Kigoma jana march 12, ilifanya ziara Manispaa ya Kigoma/Ujiji kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama huku wakiwaasa Wataalamu wa Halmashauri hiyo kutozarisha kero na kuwasumbua wananchi katika utoaji wa huduma
Aliyasema hayo Katibu Mkuu wilaya ya Kigoma wa Chama hicho Ndugu. Jumanne Kitundu alipokuwa katika kukagua miradi iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa kwa kipindi hiki cha serikali ya Awamu ya Tano
Alisema katika utendaji kazi wa watumishi wa serikali zipo taarifa za baadhi ya watumishi kutotoa huduma kwa wananchi kwa uzuri hivyo watumishi hao kutumia lugha zisizositahiri katika maeneo yao ya kazi na kuleta huduma mbovu serikalini na wengine kuzalisha matatizo au kero kwa wananchi
Aliendelea kusema “Ninyi watumishi mnapaswa kuwa waamifu katika kazi zenu za kila siku mnazozifanya, na taarifa tunazo kwa wasiowaamifu na mnaotoa lugha zisizo sahihi na wengine kutumia mda mwingi bila sababu kutoa huduma jambo ambalo halikubaliki, Niwatake ninyi kama Watumishi tumieni maadili yenu ya kazi kufanya kazi kwa uaminifu ili tufike pale tunapotarajia kufika kama Watanzania”
Wakiwa katika eneo la Mlima Masanga ambapo ni chanzo cha mapato cha madini ya Manispaa hiyo Afisa Mapato Ndugu . Amoni Ndakize alitoa taarifa na kueleza kuwa chanzo hicho kwa mwaka 2019 kimeingiza zaidi ya Fedha za Kitanzania Shilingi Millioni Moja(1,000,000/=) licha ya changamoto ya namna watoza ushuru wanavyokusanya kutokana na ukubwa wa mlima huo
Wakiwa katika kitalu cha michikichi eneo la Katosho Mkuu wa idara ya Kilimo, Ushirika na Umwagiliaji Ndugu. Haruna Mtandanyi akitoa taarifa alisema kwa sasa Manispaa imejikita katika uzalishaji wa miche ya michikichi kutokana na sera ya kuinua zao hilo na kusema lengo la kuzalisha miche milioni moja laki saba na elfu hamsini(1,750,000) ambapo michikichi hiyo itagawiwa kwa wananchi pasipo gharama yeyote
Aliendelea kusema hadi sasa miche elfu kumi na moja (11,000) tayari ipo katika viliba na mbegu zaidi ya elfu thelathini(30,000) zimesha zalishwa katika vitalu ili kuweza kuhamishia katika vitalu ambapo hadi kufikia mwezi Desemba, 2020 miche hiyo itakuwa tayari kusambazwa kwa wananchi na wakulima ambapo itakuwa na uwezo wa kuzalisha Tani 4 za mafuta ya mawese kwa hekari kwa mwaka tofauti na michikichi ya sasa yenye uwezo wa kuzalisha Tani 1.5 kwa hekari kwa mwaka
Aidha wajumbe hao wa kamati ya siasa wakitoa maoni yao katika ziara waliyoifanya, Katibu Mwenezi wa wilaya (CCM) Ndugu. Haruna Kambilo ameipongeza serikali ya Awamu ya Tano kwa kuendelea kuleta miradi mbalimbali katika Manispaa hiyo na kuwapongeza wasimamizi ambao ni wataalamu
Aliendelea kutoa ushauri kuwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji katika ukusanyaji mapato ihakikishe pia inarudisha maendeleo kwa kuboresha miundombinu katika vyanzo inavyokuwa inakusanya huku akitaka katika uchimbaji wa madini mlima wa Masanga kuweka miundombinu imara ya barabara ya kuwezesha usafirishaji na kuwapa mikopo wachimbaji hao ya vifaa vya uchimbaji
Kaimu mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu.Frednand Filimbi katika ziara hiyo aliipongeza kamati ya siasa ya chama hicho kwa ziara waliyoifanya huku akiahidi kutekeleza ushauri walioutoa na kuendelea kutekeleza na kusimamia ilani ya Chama hicho
Katika ziara hiyo miradi mingine iliyotembelewa ni pamoja na ukarabati wa shule ya sekondari Lubengera unaoendelea, Machinjio ya Kibirizi na Ujiji, Soko la samaki la Kibirizi, Dampo la Kisasa Msimba,barabara 8 zilizojengwa chini ya mradi wa TSCP zenye urefu wa Km 11.97, eneo la soko la samaki soko la Kigoma mjini, ujenzi wa Zahanati unaoendelea eneo la Buronge, Makumbusho ya Dr.Living stone Ujiji, stesheni ya Kimoja, na barabara ya Katonga inayoendelea kujengwa kwa kiwango cha lami.
ingia katika maktaba ya picha kuona picha zaidi ya ziara hiyo
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa