Katibu wa chama cha mapinduzi (ccm) mkoani kigoma Ndugu.Dastani Shao jana novemba 1, 2018 ametembelea miradi ya maendeleo katika manispaa ya Kigoma Ujiji na kuwataka wataalamu wa manispaa kusimamia miradi ambayo haijakamilika na kukamilika katika viwango vinavyokubalika.
Katika ziara hiyo katibu wa chama hicho mkoa wa kigoma aliongozana na kamati ya siasa na sekretariati mkoa , viongozi wa chama cha mapinduzi wilaya, pamoja na wataalamu wa halmashauri hiyo kutoka ofsi ya mkurugenzi.
Ziara hiyo ilianza kutembelea mradi wa ujenzi wa barabara ya kagashe inayojengwa kwa kiwango cha lami ambapo mhandisi wa manispaa Eng. Wilfred Shimba alitoa taarifa ya barabara zote zinazojengwa katika manispaa ya kigoma ujiji takribani barabara 7,ikiwemo na kipande cha barabara katika hospitali ya maweni, na ujenzi wa mfereji wa maji ya mvua katonyanga, mhandisi huyo aliendelea kusemba tayari baadhi ya barabara zmefika katika kiwango kizuri cha G15 katika ujenzi huo , barabara hizo ikiwa ni barabara ya Kagashe, barabara ya mawen-burega,mwanga-kitambwe-mwembetongwa, ujenzi-nazareth, barabara ya kaaya-simu,kakolwa na mfereji wa katonyanga, mhandisi huyo ameendelea kusemamesema ujenzi huo wa miradi hiyo utachukua miezi 15hadi kukamilika na umeanza julai 06, 2018 na unatarajia kukamilika octoba 06, 2019.
Baada ya ukaguzi wa barabara hizo ziara iliendelea kukagua mradi wa maji uliopo eneo la mgumile ambapo mhandisi Eng. Wilfred Shimba aliendelea kutoa taarifa ya tanki lililojengwa na majengo yaliyojengwa eneo la chanzo cha maji hayo, mhandisi huyo alisema mradi huo utagharimu million 529 hadi kukamilika ikiwa chanzo cha fedha ni kutoka benki ya dunia(WB) ambapo mradi huo utahudumia zaidi ya watu 2000 wanaoishi eneo hilo la Mgumile, lakini pia ukaguzi umefanyika katika jengo la zahanati la mgumile lililogharimu million 58, ambapo miradi yote hiyo miwili mradi wa maji na jengo la zahanati viongozi na kamati ya siasa ya CCM ikiongozwa na katibu wa chama hicho hawakulidhishwa na miradi hiyo iliyojengwa.
Ziara hiyo imeendelea kwa kukagua ujenzi wa jengo la madarasa katika shule ya msingi Kigoma, ukarabati wa majengo katika zahanati ya Kigoma mjini na ujenzi wa daraja eneo la kilimahewa , katika ukaguzi wa jengo la madarasa jengo hilo likiwa na vyumba vya madarasa tisa(9) ambapo linatarajia kugharimu million 218, ikiwa ujenzi huo umefadhiliwa na ubalozi wa serikali ya Japan ambapo ujenzi huo unatarajia kukamilika novemba 20,2018.
Wakiwa katika zahanati ya Kigoma mjini taarifa ya ukarabati wa majengo ilitolewa na mkuu wa kituo hicho ambapo aliweza pia kueleza changamoto zinazoikabili kituo hicho ikiwa ni pamoja na ukosefu wa hati ya kiwanja hicho wanachofanyia kazi, wahudumu wachache, na ufinyu wa wodi ya wazazi.
Ziara ilikamilika katika barabara ya Dr. mzazi katika kukagua ujenzi wa daraja liliojengwa chini ya usimamizi wa TARURA ambapo alitoa taarifa ya ujenzi wa mradi huo na taarifa kupokelewa na katibu wa CCM mkoani Kigoma.
Wakiwa katika kikao cha majumuisho ya ziara hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa manispaa katibu wa chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kigoma akiwa na kamati ya mkoa walitoa mtazamo na maoni ya miradi waliyozungukia.
Katibu huyo alianza kwa kushukuru ofsi ya Mkurugenzi manispaa na timu nzima ya wataalamu iliyoambatana naye na kusema kuna miradi inayoendelea kujengwa kama barabara na madarasa yaendelea kusimamia vizuri ikiwa imejengwa kwa kiwango kizuri , na aliendelea kupongeza mradi wa ukarabati wa majengo katika kituo cha zahanati ya Kigoma mjini na ujenzi wa daraja la kilimahewa barabara ya Dr.mzazi. licha ya kupongeza miradi hiyoalisema hajaridhishwa na mradi wa maji Mgumile ambapo alisema majengo katika chanzo hicho yamejengwa bila kuwa na msingi wa kutosha ili kuepuka maji kujaa katika jengo hilo kipindi cha mvua, lakini pia katika kukagua ujenzi wa jengo la zahanati kiongozi huyo alishauri mhandisi aliyejenga jengo hilo atafutwe kutokana na ujenzi wa jengo hilo kuwa chini ya kiwango na kutumia gharama kubwa million 58 katika ujenzi wa jengo hilo.
Naye kaimu afisa Uchumi Ndugu. Robert Sabhoya kwa niaba ya mkurugenzi ameshukuru uongozi mzima wa chama cha mapinduzi mkoa na wilaya kwa ziara iliyofanyika na kusema ushauri uliotolewa wataendelea kuufanyia kazi kupitia vikao vyote vinavyofanyika chini ya mkurugenzi.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa