Na Mwandishi Wetu
Wajumbe wa Kamati ya Mpango wa Taifa wa Kupinga ukatili wa Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) Manispaa ya Kigoma Ujiji Jana Desemba 31, 2024 ilifanya kikao katika ukumbi wa Manispaa hiyo.
Kikao hicho kilifanyika kikifadhiliwa na taasisi ya BAKAIDS kwa lengo la Wajumbe kukumbushana Wajibu wa kuendelea kupinga ukatili ndani ya Jamii kwa kutoa taarifa na elimu kwa makundi mbalimbali.
Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao hicho Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo Majira Jabiri alisema Wajumbe wa Kamati ya MTAKUWWA Kila mmoja ana Wajibu wa kutumia taalamu na elimu aliyonayo ili kuendelea kuisaidia jamii kuenenda katika maadili yanayokubalika na katika malezi ya Watoto.
Kamati ya MTAKUWWA inaundwa na Wadau mbalimbali wakiwemo Jeshi la Polisi, Maafisa Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Afisa Elimu, Maafisa biashara, Viongozi wa dini, Wadau na Viongozi mbalimbali.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa