Na Mwandishi Wetu
Kamati za maafa ngazi ya Kata na Mitaa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Leo March 25, 2025 zimepata mafunzo ya kujengewa uwezo juu ya masuala ya kuimarisha ufuatiliaji na udhibiti wa Majanga katika maeneo yao.
Mafunzo hayo yametolewa na Maafisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu (Idara ya Menejimenti ya Maafa) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia uhamaji (IOM) katika Ukumbi wa Redcross.
Mafunzo hayo yamehudhuriwa na Watendaji Kata, Watendaji wa mitaa, na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kutoka katika Kata ya Kitongoni, Buzebazeba, Kagera, Kibirizi, Bangwe, Businde, na Katubuka.
Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mkuu wa Idara ya udhibiti taka na Usafi wa Mazingira Bi.Petronila Gwakila amesema mafunzo hayo yatawasaidia kutambua namna ya kukabiliana na kudhibiti Majanga pale yanapotokea katika maeneo yao.
Amesema Manispaa ya Kigoma/Ujiji imekuwa ikikumbwa na mafuriko katika baadhi ya maeneo, Kuongezeka kwa maji katika Ziwa Tanganyika, na uwepo wa Wanyama hatarishi kando ya Ziwa hali ambayo imekuwa ikileta madhara makubwa kwa Wananchi.
Mratibu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Idara ya Menejimenti ya Maafa Naibu Kamishina Hamisi Rutengo amesema mafunzo hayo ni kujengeana uwezo namna ya kukabiliana kabla ya tukio kutokea, wakati wa tukio kutokea, na baada ya tukio kutokea ili kupunguza madhara kwa Wananchi.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa