Na Mwandishi Wetu
Kampeni ya msaada wa kisheria ( Samia Legal Aid ) iliyozinduliwa Januari 24,2025 imefanikiwa kuwafikia Wananchi na Wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji zaidi ya Watu elfu arobaini na saba (47, 636) iliyofanyika kwa mda wa Siku kumi (10).
Msaada wa kisheria uliyotolewa bure kwa Wananchi ikiwa ni maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan ukilenga kutoa elimu na utatuzi wa migogoro katika maeneo tofauti tofauti ikiwemo Migogoro ya ardhi, Ukatili wa kijinsia, mirathi, ndoa na masuala ya uraia.
Timu ya Wataalamu wa kampeni ya msaada kisheria ya Mama Samia ya Manispaa ya Kigoma Ujiji (Mama Samia Legal Aid Campaign) ikitoa taarifa Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Leo Februari 03, wamesema zoezi hilo lilihitimishwa Jana Februari 02, 2025.
Wamesema Migogoro mia mbili sabini na tano (275) iliyohusu migogoro ya ardhi, ndoa, mirathi, ukatili wa Kijinsia, madai, na jinai iliipokelewa na kutatuliwa katika Kata kumi (10) zilizofikiwa na Wataalamu hao.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa