Na Mwandishi Wetu
Katibu tawala wa Mkoa wa Kigoma Leo Desemba 21, 2021 amewataka wakazi wa Mkoa huo kujenga tabia ya kuripoti vitendo vya ukatili vinavyoweza kutokea ndani ya jamii
Ameyasema hayo katika uzinduzi wa Mwongozo wa kampeni ya kupinga ukatili iliyofanyikia Ukumbi wa Redcross Manispaa ya Kigoma/Ujiji ikienda kwa jina la Twende Pamoja ukatili Kigoma sasa basi
Akihutubia katika ukumbi huo amewataka wakazi wa Mkoa huo kuwa na tabia itakayosaidia kutokomeza vitendo vya ukatili katika jamii kwa kutoa taarifa katika taasisi za Serikali kama vile Dawati la Jeshi la Polisi, Ofisi za Ustawi wa Jamii, Ofisi za Kata na Mitaa ili kutokomeza vitendo hivyo
Katibu tawala huyo ameyataka Mashirika ya Serikali na yasiyo ya Serikali kuendelea kuelimisha jamii kupitia makundi ya watu wengi na vyombo vya habari ili kuwa na jamii yenye Mazingira yaliyo salama katika shughuli za Kiuchumi za kila siku
Aidha amewataka Wazazi na Walimu kusimamia maadili ya watoto na kuwaepusha na maudhui ya mitandao ya kijamii yasiyokuwa na maadili ambayo yanaweza kusababisha ukatili na vitendo viovu ndani ya jamii
Amewataka viongozi wa dini kuendelea kuelimisha waumini kuwa na hofu ya Mungu na kuepukana na vitendo ambavyo ni kinyume na maadili ya jamii huku waganga wa jadi wakitakiwa kufanya kazi kwa uaminifu na kutokutoa maelekezo yanayoleta athari ya vifo na maumivu ndani ya jamii
Aidha amezitaka Halmashauri za Mkoa wa Kigoma kuimarisha kamati za Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwa Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) na kuwa na vikao vya Mara kwa Mara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kutokomeza vitendo hivyo vya ukatili
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia- Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Mwajuma Magwiza amesema katika Mwongozo uliozinduliwa mambo yanayosisitizwa ni pamoja na Kuimarisha Uchumi wa Kaya, jamii kuepuka Mila na desturi potofu na kuweka Mazingira salama Mashuleni na Majumbani kwa watoto na wanafunzi
Ameendelea kusema Mpango wa MTAKUWWA una lengo la kupunguza vitendo vya ukatili hadi kufikia asilimia Hamsini (50%) huku akisema anaamini mwongozo wa kampeni ya Twende pamoja kupinga Ukatili Kigoma kama ukitumiwa kikamilifu utasaidia kutokomea kwa vitendo hivyo Nchini
Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Kigoma Ndugu. Elisha Nyamara amesema tangu Mwaka 2018 ambapo Mpango wa Kupambana na Vitendo vya ukatili wa Kijinsia na watoto ulipozinduliwa jumla ya Askari Mia moja kumi na tano (115) wamepatiwa mafunzo ya kupambana na vitendo vya ukatili, wahanga wa vitendo vya Ukatili elfu moja Mia moja kumi na nne (1114) wakipatiwa msaada na usaidizi na kisheria huku wataalamu wa afya Mia moja na thelathini (130) wakipatiwa mafunzo namna ya kuwahudumia waathrika na vikao vya kamati ya MTAKUWWA vikifanyika kila mwaka
Nao baadhi ya washiriki wa Semina hiyo Mwalimu Gervas Rwaho na Mjasiriamali Bi. Beatrice Mtesigwa wamesema jamii ina amejibu wa kufuatilia vitendo vya ukatili na kukemea ili kuwa na jamii yenye iliyo sitarabika
Mkutano huo Umehudhuria na wadau mbalimbali wakiwemo Viongozi wa dini, Wanazuoni, waganga wa Jadi, Wazee na Viongozi Maarufu, Makundi ya Wanawake na vijana, Jeshi la Polisi , vikundi vya sanaa, walimu wa Msingi na Sekondari , waandishi wa Habari na watumishi wa idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa