Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba Leo March 07, 2025 amezindua kampeni ya upandaji miti 150 kwa kila Shule ya Msingi Kata ya Katubuka.
Kampeni hiyo imezinduliwa Shule ya Msingi Majengo kwa kupanda miti ikienda sambamba na uzinduzi wa mpango mkakati rekebishi wa ufuatiliaji na tathimini ya elimu kwa Miaka mitatu (2025-2028) katika Kata hiyo.
Afisa elimu Kata ya Katubuka Ndugu. Jovitus Augustus akiwasilisha taarifa amesema mpango huo unalenga kukuza ufaulu wa Wanafunzi katika Kata hiyo.
Amesema mpango huo umeainisha mkakati wa ufuatiliaji wa Walimu na Wanafunzi watoro, kuweka mkakati wa Wanafunzi wasiomudu stadi za kusoma, kuhesabu na kuandika (KKK), Utunzaji wa Mazingira, na Ustawi wa Wanafunzi kwa kuwalinda na kupinga vitendo vya ukatili.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa