Na Mwandishi Wetu
Manispaa ya Kigoma/Ujiji Leo Octoba 6, 2023 imefanya maadhimisho ya juma la Elimu la Watu Wazima lililofanyikia Shule ya Sekondari Mwananchi.
Maadhimisho hayo yamefanyika yakiongozwa na Mgeni Rasmi Afisa elimu Watu Wazima Mkoa wa Kigoma Ndugu. Hawamu Tambwe na kuhudhuliwa na Wataalamu kutoka Taasisi ya Elimu, Ofisi ya Mkuruģenzi, Walimu, Wanafunzi na Wananchi mbalimbali.
Maadhimisho hayo yamefanyika yakiambatana na shuhuda za elimu ya jamii kutoka kwa Wanafunzi wa elimu ya Sekondari kwa njia mbadala (SEQUIP-ASEP) Shule ya Sekondari Mwananchi.
Manispaa ya Kigoma/Ujiji imeendelea kutoa elimu kwa Wanafunzi Watu wazima kupitia elimu ya Sekondari kwa njia Mbadala (SEQUIP-ASEP) katika Kituo cha Shule ya Sekondari Mwananchi na katika Vituo vya MEMKWA kumi na nane (18) kwa Shule za Msingi.
Juma la Elimu Watu wazima huadhimishwa Duniani kuanzia Septemba 01-08, Kila Mwaka na kwa Mwaka huu Kauli mbiu ni " kukuza uwezo wa kusoma na kuandika kwa ulimwengu unaobadilika, kujenga misingi ya Jamii endelevu na yenye Amani".
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa