Na Mwandishi Wetu
Maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania bara yamefanyika Manispaa ya Kigoma/Ujiji yakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr. Rashid Chuachua kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa kwa kufanya Usafi na upandaji Miti katika Hospitali ya Manispaa hiyo iliyopo Kata ya Kagera.
Zoezi la usafi na upandaji miti limefanyika na Viongozi Serikali, Siasa na Wananchi ambapo Mkuu wa Wilaya amewataka Wananchi kuendelea na utunzaji wa mazingira.
Akizungumza mara baada ya Zoezi hilo Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Ndugu. Hassani Rugwa amewapongeza Wananchi kujitokeza katika Sherehe za Maadhimisho huku akiwataka Wananchi kuendelea kulinda amani na Utulivu uliopo na kusema Serikali inaendelea kutekeleza miradi ya Maendeleo ya zaidi ya Trillion 11.5/= Mkoani hapo.
Kauli Mbiu ya Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania bara ni " Uongozi Madhubuti na Ushirikishwaji wa Wananchi ni Msingi wa Maendeleo yetu".
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa