Na Mwandishi Wetu
Hashauri ya Manispaa ya Kigoma/ Ujiji imesaini Mkataba na Benki ya CRDB kwa ajili ya utoaji mikopo isiyokuwa na riba kwa makundi ya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu.
Hafla hiyo imefanyika baina ya Viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji na uongozi wa Benki ya CRDB katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma yakishuhudiwa na Waziri wa OR-TAMISEMI Mhe. Mohammed Mchengerwa.
Mikataba hiyo imesainiwa kwa Halmashauri kumi (10) ili kuwahudumia Wananchi kikamilifu kupunguza umasikini na kujiongezea kipato.
Halmashauri zingine zilizosaini Mikataba ni pamoja na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam, Jiji la Dodoma, Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Halmashauri ya Bumbuli, Halmashauri ya Wilaya ya Siha, Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu na Halmashauri ya Itilima.
Zaidi bofya www.kigomaujijjmc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa