Ni mwaka mmoja sasa tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuapishwa kwake March 19, 2021 kuwa Rais wa Nchi baada ya kifo cha aliyekuwa Rais Mhe. John Pombe Magufuli alipofariki March 17, 2021
Mara baada ya Kuapishwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alianza kutekeleza na kusimamia miradi mbalimbali Nchini Kupitia Wizara na Taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kulinda Katiba ya Nchi
Kwa kipindi cha Mwaka Mmoja cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameendelea na utekelezaji wa shughuli za Serikali na usimamiaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Wizara mbalimbali na kufanya Mikoa na Halmashauri kunufaika na miradi ya maendeleo kutokana na mapato ya ndani, fedha za wahisani na fedha kutoka Serikali Kuu
Wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji ni miongoni mwa wanufaika wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka mmoja wa Awamu Sita ikiwa ni pamoja na Ustawi wa Jamii katika sekta mbalimbali
SEKTA YA ELIMU
Katika sekta ya Elimu zaidi ya Tsh Billion 2 zimepokelewa Manispaa ya Kigoma/Ujiji katika kipindi hiki cha mwaka mmoja wa Awamu ya Sita kwa idara ya Elimu Msingi na Sekondari
Idara ya Elimu Msingi Manispaa ya Kigoma/Ujiji imepokea zaidi ya Tsh Million 260 ili kutekeleza miradi ambapo kiasi cha Tsh 180,000,000/= zimetumika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa tisa(09) katika Shule za Msingi Benjamini Mkapa (2) , Butunga (2), Mwasenga (2), Mlole (2) na shule ya Msingi Kipampa (1)
Aidha utekelezaji huo umeendelea kwa ujenzi wa matundu ya vyoo sitini (60) kwa kiasi cha Tsh 66,000,000/= kwa Shule za Msingi Mlole (6), Mwasenga (6), Butunga (12), Kiheba (12), Majengo (12) na Shule ya Msingi Mwasenga (12)
Mradi mwingine uliotekelezwa kwa Idara ya Elimu Msingi ni wa kujikinga na kupambana na athari za Uviko-19 kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi ambapo Zaidi ya Tsh Miillion 20 zilitumika kujenga miundombinu ya ujenzi wa kunawa mikono kwa Walimu na Wanafunzi Shule ya Msingi Mwasenga na Butunga zilizopo katika Manispaa hiyo
Idara ya elimu Sekondari Manispaa ya Kigoma/Ujiji Kwa kipindi cha Mwaka mmoja cha Mhe. Rais imepata fedha za miradi ya maendeleo Zaidi ya Billion 2 jumla ya madarasa hamsini na tisa (59) yamejengwa ambapo Madarasa arobaini na nane (48) yamejengwa kwa Shule mbalimbali na kukamilika kwa kiasi cha Tsh 960,000,000/= katika mradi wa kupambana na athari za Uviko-19 ambapo ulifanikiwa kutoa ajira 414 na kuwanufaisha Wanafunzi 2400 ambapo hadi sasa madarasa yanatumika, na ujenzi wa madarasa nane (08) katika Shule za Sekondari Buronge (02), Bushabani (02), Masanga (02) na Shule ya Sekondari Gungu (02)
UJENZI WA SHULE MPYA YA SEKONDARI
Aidha kwa kipindi hiki cha mwaka mmoja Cha Utawala wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan fedha ya awali kwa ajili ya Ujenzi wa Shule mpya katika kata ya Businde imetolewa kiasi cha Million 470/= na Shule hiyo inatarajia kukamilika kwa kiasi cha Millioni 600/= ambapo awali Kata hiyo haikuwa kuwa na Shule ya Sekondari, miradi mingine ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa Maabara kwa Shule za Sekondari kumi na moja (11) kwa gharama ya Tsh Million 330/= na ujenzi wa matundu ya vyoo kumi na moja (11) kwa shule ya Sekondari Masanga
SEKTA YA AFYA
Katika Sekta ya Afya, kwa kipindi cha Mwaka mmoja cha Utawala wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan Manispaa ya Kigoma/Ujiji imepokea zaidi ya Tsh Million 610/= ambapo kiasi cha Tsh 250,000,000/= tayari imepokelewa kwa lengo la ujenzi wa Zahanati ya Buhanda ikiwa ni fedha ya awali na kituo hicho kinatarajia kukamilika kwa Tsh Million 600/= ikiwa ni fedha kutokana na tozo ya Miamala ya Simu
Fedha zingine zilizopokelewa kutoka Serikali Kuu ni Tsh 250,000,000/= za ujenzi wa jengo la Wagonjwa wa Nje (Opd) katika kituo cha afya cha Gungu, ujenzi wa uzio katika zahanati ya Msufini kwa gharama ya Tsh million 35/=, ujenzi wa uzio wa zahanati ya Kigoma kwa gharama ya Tsh Million 35/=, ujenzi wa uzio wa Zahanati ya Buhanda kwa gharama ya Tsh Million 45/=, na ujenzi wa uzio wa zahanati ya Businde kwa gharama ya Tsh Million 45/= ambapo kukamilika kwa ujenzi huo kutasaidia ulinzi katika maeneo ya vituo hivyo, upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi na haraka
MIUNDOMBINU YA BARABARA
katika uboreshaji wa miundombinu ya barabara Serikali ya Awamu ya Sita ikiongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kipindi cha Mwaka mmoja Manispaa ya Kigoma/Ujiji chini ya usimamizi wa TARURA imepokea zaidi ya Billion 2 na kuongeza Mtandao wa barabara kutoka Km 324 zilizokuwepo awali na kufikia Km 336.51 hadi hivi sasa
Aidha Serikali Kuu imetoa kiasi cha Tsh Billion moja (1, 000,000,000/=) ambapo zimetumika katika ujenzi wa barababara ya Mabatini na Muungano B kwa kiwango cha lami ambapo jumla ya Km 0.8 zimejengwa, ujenzi wa barabara ya Muungano Km 2.01 ( starehe-Kilimahewa), na barabara ya Mlimani 0.5 km na Mitalo kwa kiwango cha changarawe
Fedha zingine ni Billion 1. 05 zimeendelea kutekeleza ujenzi wa barabara kwa matengenezo ya kawaida Km 93.3, Matengenezo ya Maeneo korofi Km 1. 56 na Matengenezo ya Mda Maalumu Km 0.63, ambapo Ujenzi wa huo wa barabara, mifereji, kalvati na Madaraja unaendelea katika Kata mbalimbali za Manispaa hiyo
HUDUMA YA MAJI
Mamlaka ya Maji Manispaa ya Kigoma/Ujiji (KUWASA) kwa kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita imefanikiwa kuongeza Mtandao wa mabomba ya Maji wenye jumla ya Km 62. 2 kwa gharama 599, 962, 060/= ambapo hadi sasa kiasi cha Tsh Million 200/= imepokelewa kwa ajili ya ununuzi wa bomba na vifaa vya km 18 katika maeneo ya Busomelo, Kagera, Kigamboni, Bushabani, Kibirizi, Bangwe na Buronge na inatarajiwa kufanyika Kilimahewa, na Gungu
ANWANI ZA MAKAZI
Manispaa ya Kigoma/Ujiji tayari imepokea zaidi ya fedha Kiasi cha Million 97/= kutoka Serikali Kuu kwa lengo la utekelezaji wa mradi wa Anwani za Makazi ambapo hadi hivi sasa Utekelezaji huo unaendelea na mradi huo utasaidia Kila Mkazi wa Manispaa hiyo kutambuliwa na kurahisisha upatikanaji wake , uwekaji wa Namba za Nyumba, Majina ya Mtaa na Postikodi ambapo kukamilika kwake kutusaidia kukuza na kuboreshwa kwa huduma za Ulinzi na Usalama ndani ya Jamii, kufanyika na kukuza kwa biashara Mtandaoni kidigitali na Kusaidia Serikali kufikisha huduma kwa wananchi kirahisi kulingana na Mahitaji ya eneo husika
MRADI MPYA
Mradi mwingine unaotarajia kutekelezwa ni wa kuendeleza na Kukuza Miji na Majiji Kimkakati (TACTICs) ambapo ujenzi wa barabara mbalimbali kwa kiwango cha lami unatarajiwa kufanyika Manispaa ya Kigoma/Ujiji ambapo zaidi ya Km 15 zinatarajiwa kujengwa, Ujenzi wa Kisasa soko la Mwanga, Ujenzi wa Kisasa wa Soko la mazao ya Uvuvi Katonga, Ujenzi wa miundombinu ya Mifereli ya Maji ili kudhibiti athari zitokanazo na mmomonyoko ambapo Mtalo Burega, Bushabani, Mji Mwema, Katonyanga na Mlole mifeji hiyo inatarajiwa kujengwa ili kudhibiti athari kwa Wananchi
Hivi Karibuni Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akihojiwa na baadhi ya vyombo vya habari vikiangazia Utekelezaji wake kwa kipindi cha Mwaka mmoja wa Utawala wake alisema ataendelea na Utekelezaji wa Miradi Mbalimbali ya Kimaendeleo ili kukuza Uchumi wa Nchi, Kuzalisha ajira na kuongeza Ustawi wa Maisha ya Watanzania katika kipindi chote cha Utawala wake
Picha na ya miradi mbalimbali iliyotekelezwa inapatikana katika maktaba ya picha kupitia tovuti ya www.kigomaujijimc.go.tz na mitandao yetu ya kijamii
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa