Na Mwandishi Wetu
Serikali ya Tanzania Leo Oktoba 11, 2023 imetia saini Mikataba mitatu na Kampuni ya Dearsan Shipyard ya Nchini Uturuki wa Ujenzi wa meli kwa ziwa Tanganyika na ziwa Victoria kwa gharama ya Zaidi ya Billion 630.
Utiaji wa Saini huo umefanyikia katika eneo la Bandari Mkoani Kigoma na zoezi hilo likishuhudiwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Profesa Makame Mbarawa, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Bandari Nchini Tanzania, Wabunge, Viongozi wa vyama vya Kisiasa, Wananchi na Waandishi wa habari
Kusainiwa kwa mikataba hiyo kunahusisha Ujenzi wa kiwanda cha ujenzi wa meli (karakana) ya kudumu katika Ziwa Tanganyika ambapo itajengwa chererezo yenye uwezo kubeba Meli ya uzito wa Tani 5000 kwa gharama ya fedha za Kitanzania Billion 322.7 Ujenzi ukitekelezwa kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia sasa.
Aidha kusainiwa kwa mikataba hiyo kunahusisha Ujenzi wa meli ya mizigo Ziwa Tanganyika yenye uwezo wa kubeba Tani 3500 ambayo ni meli kubwa kuliko zote ukanda wa maziwa Makuu ambayo itakuwa na uwezo wa kusafiri kupitia bandari za Burundi hadi bandari ya Kalemi Nchini Congo kwa mda wa Masaa sita.
Katika Mkataba hiyo iliyosainiwa imehusisha Ujenzi wa Meli ziwa victoria yenye uwezo wa kubeba Tani 3000 kwa gharama ya fedha za Kitanzania Billion 145 na itajengwa kwa mda wa miaka miwili.
Zaidi www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa