Na Mwandishi wetu.
Naibu waziri wa Tamisemi Mhe. Josepahati Kandege leo may 9, amezindua kongamano la uwekezaji mkoani Kigoma linalozungumzia fursa mbalimbali zilizopo mkoani hapo.
Katika kongamano hilo liliofanyika katika ukumbi wa NSSF halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji wadau mbalimbali wamehudhulia wakiwemo wawakilishi kutoka nchi jirani nchi ya Burundi, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Rwanda na Zambia ambapo wawakilishi kutoka mikoa jirani nayo wamehudhulia , mkoa wa Katavi na Kagera.
Akimkaribisha mgeni rasmi mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emmanuel Maganga alianza kwa kuwatakia pole Watanzania wote kwa msiba mkubwa uliolikumba Taifa kwa kifo cha Dr. Reginard Mengi.
Mkuu wa mkoa huyo amewakaribisha wadau mbalimbali kutoka mkoa wa katavi, kagera na wawakilishi kutoka nchi jirani huku akisema Kigoma ni eneo salama kiuwekezaji na nchi jirani ambazo zilikuwa na migogoro ya kisiasa, migogoro hiyo imepungua.
Akizindua kongamano hilo Naibu waziri wa Tamisemi kwa niaba ya Makamu wa raisI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu amesema kongamano hilo ni la kwanza na la kitaifa ambalo kwa jina la Tanganyika Bussines Summit and Festival na kushukuru ofsi ya mkuu wa mkoa na Chamber ya Kibiashara (TCCIA), Local Investimate Climate( LIC) na wadau wengine kwa kufanikisha maandalizi ya mkutano huo.
Amewataka wadau mbalimbali waliohudhulia kongamano hilo kuona fursa zilizopo mkoani hapo na mkutano mkubwa huo kuwanufaisha na kuhakikisha kushiriki kikamilifu ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu wa kibiashara baina ya wafanyabiashara wa Tanzania na wafanyabiashara wan chi zinazozunguka ziwa Tanganyika.
Akizungumza katika kongamano hilo fursa zilizopo mkoani Kigoma Mshauri Mwelekezi wa uwekezaji Ndugu. Osward Mashindano amesema “K igoma ina fursa nyingi na utajiri wa kutosha lakini bado wananchi sio matajiri na fursa hizo baadhi ya watu hawazifahamu”
Ameendelea kusema Kigoma ina wakazi zaidi ya milioni 2 jambo linalofanya kuwepo na soko la uhakika kibiashara na uwepo wa nguvu kazi katika masuala ya uwekezaji , ambapo amewakaribisha wadau mbalimbali wa ndani na nje kuja kuwekeza mkoani hapo.
Ameendelea kusema mkoa wa Kigoma una madini tofauti tofauti aina kumi jambo linalovutia wawekezaji katika soko hilo na hadi hivi sasa kuna masoko makubwa manne(4) yaliyoanzishwa masoko 2 yakiwa wilaya ya Kankonko, soko 1 likiwa wilaya ya Buhigwe na soko lingine likiwa wilaya ya Kigoma.
Ameendelea kusema tayari mkoa umetenga eneo la uwekezaji kwa jina la Kigoma development economic zone ambapo wawekezaji walishapewa maeneo na baadhi wameanza kujenga miundombinu mbalimbali ya viwanda vya uchakataji wa mafuta ya mawese na korie ,na mitambo ya umeme
Amehitimisha kwa kuwataka wadau mbalimbali kuja kuwekeza mkoani hapo katika kilimo cha miwa katika bonde la mto Ruiche, kilimo cha ufugaji nyuki kutokana na misitu iliyopo mkoani hapo wilaya ya Kibondo na kasulu na kuja kuja kufanya utalii katika hifadhi ya Mbunga ya Mahare na hifadhi ya Gombe, kuwekeza katika ufugaji na uvuvi wa samaki kutokana na uwepo wa ziwa Tanganyika na kuwekeza katika usafirishaji wa majini, nchi kavu na anga.
Aidha katika uzinduzi wa kongamano hilo umeenda sambamba na uzinduzi wa kitabu kinachozungumzia fursa zilizopo mkoani Kigoma, kongamano linatarajiwa kufanyika kwa mda wa siku tatu kuanzia mei 9 hadi mei 11 katika kongamano hilo lililoandaliwa na ofisi ya mkoa wa kigoma na washiriki wakiwa ni wadau kutoka nchi na mikoa inayozunguka ziwa Tanganyika. .
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa