Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba amesema kwa sasa ujenzi unaoendelea kwa Shule za Sekondari ni wa madarasa ya ghorofa.
Ameyasema hayo Leo Novemba 25, 2025 katika kipindi cha #GoodmorningKigoma kinachorushwa na Radio Joy iliyopo katika Manispaa hiyo.
Amesema ujenzi wa madarasa ya ghorofa unafanyika kutoka na ufinyu wa ardhi katika maeneo ya mjini na hadi sasa Ujenzi wa huo umeshafanyika Shule ya Sekondari Mji Mwema, na unaendelea Kata ya Kipampa na Burega ukiwa unaendelea.
Amesema kwa sasa zaidi ya Billion 4 zinatekeleza ujenzi wa miundombinu kwa Shule za Msingi na Sekondari na tayari Ujenzi wa Shule za Msingi Mpya unaendelea Kata ya Kibirizi, Buhanda na Businde.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa