Na Mwandishi Wetu
Mwenyekiti wa Kamati ya Uboreshaji wa Uwanja wa Mpira wa Lake Tanganyika (Lake Tangangika Stadium) ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mhe. Salum Hamis Kali amefanya kikao na Wajumbe wa Kamati hiyo kwa lengo la kuendelea na shughuli za uboreshaji wa uwanja ili kukidhi viwango vya kuchezwa kwa mechi mbalimbali za Kitaifa ikiwemo Ligi Kuu ya Tanzania bara
Kikao hicho kimefanyika Leo July 24, 2023 Uwanjani hapo ambapo kimepokea taarifa ya Utekelezaji wa kamati ndogo ndogo zilizoundwa
Kamati hiyo inatekeleza majukumu chini ya Katibu ambaye ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Mwantum Mgonja ikishirikiana na Uongozi wa Chama cha Mpira Mkoa wa Kigoma (KRFA)
Uboreshaji wa Uwanja huo unalenga uwanja wa ndani ( Pitch na uzio), Ujenzi wa Ukuta, umwagiliaji wa eneo la michezo (Pitch), ujenzi wa urefu wa uzio, uboreshaji wa vyumba , vyoo, Majukwaa, chumba cha huduma ya kwanza na upatikanaji wa vifaa tiba
Zaidi www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa