Na Mwandishi Wetu
Maafisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Kigoma/Ujiji wametakiwa kutumia taaluma zao na kufanya kazi kwa pamoja katika kuisaidia jamii kutokana na uwepo wa changamoto za Magonjwa ya akili ndani ya Jamii
Aliyasema hayo Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Kigoma Ndugu. Petro Mbwanji Jana July 17, 2022 Wakati akifunga Mafunzo ya Siku tatu (03) kwa Watumishi Maafisa Ustawi wa Jamii wa Serikali na Mashirika binafsi katika Ukumbi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji
Alisema kwa Sasa kumekuwa na Ongezeko la Watu wenye changamoto ya afya ya akili na Magonjwa ya Akili ndani ya jamii kama vile Msongo wa Mawazo, Wasiwasi, Kujitenga, Woga, Mauaji na Watu kujiua hali inayosababisha vifo, Magonjwa na Majanga tofauti tofauti
Aidha aliwataka maafisa Ustawi wa Jamii kufanya kazi kwa pamoja na kushirikiana na wadau mbalimbali kama vile Viongozi wa dini katika kuhakikisha kunakuwa na Jamii iliyo bora na yenye watu wenye afya njema
Mkufunzi katika Mafunzo hayo ambaye pia ni Daktari wa Magonjwa ya Akili kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma (Maweni) Dr.Crensensia John aliwataka Maafisa ustawi wa Jamii kuwabaini Watu wenye changamoto ya afya ya Akili na kuwapeleka katika vituo Maalumu vya Matibabu ikiwemo Hospitali ya Mkoa Wa Kigoma (Maweni)
Naye Mratibu wa Mafunzo hayo ambaye pia ni Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Agnes Punjila alisema kumekuwa na Changamoto ya Magonjwa ya akili kwa Sasa ambayo pia yanasabibisha watu kutumia Madawa ya Kulevya, Unywaji Pombe Kupindukia, kuingia katika Kamali na kusema wako tayari kufanya kazi kama timu huku akiahidi kutoa taarifa kila robo juu ya Watu wanaohudumiwa wa changamoto za Afya ya akili na msaada wa Kisaikolojia
Miongoni mwa mada zilizowasilishwa katika Mafunzo hayo ni namna ya kuhudumia jamii katika Misaada ya Kisaikolojia, Changamoto za Kisaikolojia na Magonjwa ya Kisaikolojia
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa