Na Mwandishi Wetu
Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Manispaa ya Kigoma/Ujiji yamefanyika kwa Wananchi na wakazi kupata elimu sambamba na upimaji wa Virusi vya UKIMWI katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Mwananchi.
Akiwasilisha taarifa Mratibu wa Kudhibiti UKIMWI Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Venance Kasimo amesema maadhimisho hayo yanafanyika kwa lengo la kuongeza uelewa juu ya Kinga, Matibabu na Mwenendo wa maambukizi, kuhimiza Upimaji wa hiari, Usiri na ufuatiliaji wa huduma rafiki.
Amesema kiwango cha maambukizi Manispaa ya Kigoma/Ujiji kimeshuka hadi 0.7% ambayo ni chini ya Wastani wa 1.7% ya Kitaifa ifikapo Disemba 1, 2028 ambapo ni Wastani wa Watu wenye Virusi vya UKIMWI (MVIU) ni mtu 1 Kati ya Watu 100.
Amesema huduma za Tiba na Matunzo (CTC) zinapatikana katika vituo 11 vya afya ndani ya Manispaa ambapo WAVIU hupata huduma za afya hususani dawa za ARVs.
Akifungua maadhimisho hayo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Lawi Kajanja ameitaka
kuendelea kujenga tabia ya kupima afya ili kuzuia na kueneza maambukizi katika Virusi vya UKIMWI.
Kauli mbiu Mwaka huu ni "Shinda vikwazo, Imarisha Muitikio -tokomeza UKIMWI".
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa