Na Mwandishi Wetu
Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Kigoma ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Ndugu. Thobias Adenyenye Jana Septemba 18, ilifanya ziara ya kukagua miradi inayotarajia kutembelewa, Kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya Msingi na Wakimbiza Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2022 katika Wilaya ya Kigoma
Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa alimtaka Mkuu wa Wilaya hiyo Bi. Ester alexander Mahawe kuendelea kusimamia umaliziaji wa miundombinu ambayo bado ipo hatua ya mwisho kabla ya tarehe 22 Mwezi huu
Aidha aliwataka Wataalamu na wasimamizi wa miradi kuhakikisha nyaraka zote Mhimu zinakuwepo kwa kila mradi utakaotembelewa, kukaguliwa au kuzinduliwa na viongozi wa Mwenge wa uhuru kwa mwaka huu
Miradi iliyotembelewa na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa Manispaa ya Kigoma/Ujiji ni pamoja ujenzi wa Mtandao wa mradi wa maji uliogharimu kiasi cha Tsh 500,000,000/= , Ujenzi wa Kituo cha Afya Buhanda unaoendelea kwa gharama ya Tsh 500,000,000/=, Ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Rubuga unaoendelea kwa gharama ya Tsh 47,000,000/=
Miradi mingine ni Ujenzi wa barabara ya Mabatini na Muungano B mita 800 kwa kiwango cha lami kwa gharama ya Tsh 535,000,000/= , na ujenzi wa madarasa Manne (04) Shule ya Sekondari Buteko kwa gharama ya Tsh 80, 000, 000/=
Mwenge wa uhuru Mkoani Kigoma Unatarajia kupokelewa Septemba 28, Mwaka huu ukitokea Mkoani Katavi, Ambapo Manispaa ya Kigoma/Ujiji inàtarajia kuwa Septemba 30, 2022 Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru Mwaka huu ikiwa ni " Sensa ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo, Shiriki Kuhesabiwa Tuyafikie Maendeleo"
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa