Na Mwandishi Wetu
Baraza la Madiwani Manispaa ya Kigoma Ujiji Leo March 05, 2024 limeazimia kufanya ziara katika miradi ya Ujenzi wa barabara inayotekelezwa na Wakala wa barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).
Azimio hilo limetolewa mara baada ya Mhandisi wa TARURA Wilaya ya Kigoma kuwasilisha taarifa za utendaji kazi na Madiwani kuijadili.
Awali akiwasilisha taarifa Mhandisi kutoka TARURA Eng. Jumanne Kamuangile Amesema Wakala wa barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) inahudumia barabara Manispaa ya Kigoma/Ujiji zenye Jumla ya Km 336.51
Amesema kwa Sasa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji imeanza kutekeleza uboreshaji wa miundombinu ya barabara, Ujenzi wa Mifereji na Ujenzi wa daraja Mto Luiche kupitia mradi wa TACTIC unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.
Amesema Mtandao wa barabara za lami Manispaa ya Kigoma/Ujiji umeongezeka kutoka Km 39.48 hadi Km 50.94 huku akiainisha changamoto ya uharibifu wa Miundombinu kupitia mvua zinazendelea kunyesha, utupaji taka kwenye mifereji, kushusha vifaa vya ujenzi kama mawe, kokoto, mchanga na matofali barabarani.
Wakichangia katika Mkutano huo Waheshimiwa Madiwani wamesema kutokana na uhalibifu wa Miundombinu na changamoto za barabara kwa Wananchi wa Manispaa hiyo Wanatarajia kufanya ziara kwa kushirikiana na TARURA kwa lengo la kuona malalamiko ya Wananchi na utatuzi wake.
Bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa