Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalumu) Mhe. George Mkuchika amesema maendeleo ya Kigoma yamekuwa kwa kasi kutokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo chini Serikali ya Awamu ya Sita.
Ameyasema hayo Leo April 03, 2025 katika ziara ya kukagua na kutembelea miradi ya maendeleo Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Ameipongeza Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo imeendelea kuboresha miundombinu na kurahisisha upatikanaji wa maji, umeme, Barabara,Vituo vya afya, Hospital na Miundombinu ya Shule.
Kiongozi huyo amekagua Ujenzi wa Uwanja wa Ndege, Kukagua na kuweka jiwe la Msingi Ujenzi wa barabara ya Bangwe -Ujiji, kukagua Chanzo cha Maji Amani beach,na kukagua Ukarabati wa meli ya Mv Liemba na Sangara.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa