Na Mwandishi Wetu
Mafunzo ya kujengewa uelewa juu ya upunguzaji wa madhara ya Maafa imeendelea Leo March 26, 2025 kwa kamati za maafa ngazi ya Kata na Mitaa Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Mafunzo hayo yanaendelea ikiwa ni siku ya pili (02) yakitolewa na Wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu (Idara ya Menejimenti ya Maafa) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia uhamaji (IOM) katika Ukumbi wa Redcross.
Washiriki wa Mafunzo hayo ni Watendaji Kata, Watendaji wa mitaa, na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kutoka katika Kata ya Gungu, Kigoma, Majengo, Kasingirima, Kasimbu, Rusimbi, Rubuga, Buhanda, Mwanga Kaskazini na Mwanga Kusini.
Katika Mafunzo hayo mada zilizowasilishwa ni pamoja na Dhana ya maafa, Mfumo wa usimamizi wa maafa, tathimini ya maafa na uandaaji wa mpango wa maafa.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz @owm_tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa