Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Mwantum Mgonja Leo July 12, 2023 amefungua mafunzo ya siku nne (04) kwa Wakuu wa idara na Vitengo yenye lengo la uandaaji wa Mpango Mkakati (Stragegic Plan) wa Hamashauri kwa Mwaka 2021/2022 - 2025/2025
Mafunzo hayo yanayofanyikia ukumbi wa Kigoma Social Hall yenye lengo la kuhuisha Mpango Mkakati wa Halmashauri wa miaka mitano (05) yakiendeshwa na Mhandhiri wa Sera na Mipango kutoka chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Ndugu. Jonas Kapwani
Mpango Mkakati wa Halmashauri ni takwa la kikatiba na husaidia katika upangaji wa bajeti wa kutoa huduma kwa Wananchi, Uandaaji wa Mpango Kabambe( Master plan), uboreshaji miundombinu na Uwekaji wa mazingira wezeshi ya uwekezaji
Katika uandaaji wa Mpango Mkakati utazingatia Dira ya Taifa 2025, Mpango Shirikishi wa Mda mrefu (LTPP) 2021/2012-2025/2026 , Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano (2021/22 -2025/2026 , Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) 2020-2025, Malengo ya Maendeleo ya Dunia ( SDGs) 2030, Afican Agenda 2026, Dira ya Afrika Mashariki 2050, Muundo wa Serikali za Mitaa , na Kiongozi cha mda wa Kati cha uandaaji wa Mpango na bajeti 2008
Uandaaji wa Mpango huu utahusisha Wadau mbalimbali wakiwemo Baraza la Madiwani, Taasisi za Serikali, Taasisi zisizo za Serikali, Mashirika, Wafanyabiashara, na Wadau mbalimbali
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa