Na Mwandishi Wetu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Philip Isdor Mpango amesisitiza suala la matumizi ya nishati safi na utunzaji mazingira kwa Wananchi.
Ameyasema hayo Leo March 03, 2025 alipokuwa akifungua kongamano la maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kanda ya Magharibi yaliyofanyikia Ukumbi wa NNSF Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Amesema Serikali inatekeleza mkakati wa matumizi ya nishati safi ikiwa na lengo asilimia 80 ya Wananchi wanatumia nishati safi ya kupikia kwa kutenga fedha kwa ajili ya kupunguza gharama ya upatikanaji.
Katika hotuba yake amewataka Wanawake licha ya shughuli za kiuchumi wanazozifanya kuhakikisha wanatoa malezi ya Watoto.
Ameitaka jamii kuendelea kuepuka na kupinga vitendo vya ukatili kwa Wanawake na Watoto ikiwemo kuwanyimahaki ya urithi na umiliki wa ardhi.
Aidha amewataka kushiriki katika Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika Nchini kwa kujitokeza kugombea nafasi za Uongozi mbalimbali na kupiga Kura.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Adengenye ameishikuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuunganisha Mkoa wa Kigoma katika matumizi ya umeme wa Gridi ya Taifa, Ujenzi wa vituo vya kupoza umeme na taasisi binafsi kuwekeza katika matumizi ya umeme jua.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa