Na Mwandishi Wetu
Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kigoma leo August 5, 2021 imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi na njia pendekezwa itakayotumika katika ukimbizaji wa Mwenge wa Uhuru unaotarajia kukimbizwa katika Wilaya hiyo Septemba 27, mwaka huu
Ziara hiyo imefanyika ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Bi. Ester Alexander Mahawe ambapo jumla ya miradi tisa (09) imetetembelewa huku miradi minne (04) ikipendekezwa kuwekewa mawe ya Uzinduzi, miradi miwili (02) ikipendekezwa kuwekewa mawe ya Msingi na Miradi mitatu (03) ikipendekezwa kukaguliwa na kutembelewa na Mbio za Mwenge wa Uhuru
Miradi hiyo iliyopendekezwa Kwa Hàlmashauri ya Wilaya ni pamoja na kutembelea kiwanda kidogo cha wanawake kilichopo eneo la Kijiji cha Simbo kikijihusisha na uzalishaji Mawese, Mise, na Mafuta ya Mise na gharama ya Mradi ukiwa ni fedha za Kitanzania Million kumi na Moja na laki sita(11,600,000/=) chanzo cha fedha ikiwa ni ufadhili mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu
Aidha miradi mingine ni pamoja na Uzinduzi wa Daraja la Nyabigufa lenye gharama ya Million mia moja na saba (107,000,000/=) lilipo Mkongoro , Uzinduzi wa mradi wa Maji Kijiji cha Matyazo kilichopo kata ya Kalinzi ukiwa na gharama ya Million mia tatu kumi na saba (317,641,513/=)
Miradi mingine pendekezwa kwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji ni pamoja na Kutembelea Kitalu cha Michikichi kilichopo eneo la Katosho ambapo Jumla ya Miche laki moja na elfu kumi na sita imeshazalishwa (116,000) ikiwa imegharimu kiasi cha Million ishirini laki tano (20,500,000/=) na zaidi ya Miche elfu thelathini (30,000) imeshagawiwa kwa wakulima bure na mingine ikipandwa Kando ya barabara za mji
Miradi mingine ni Uzinduzi wa Jengo la Kujifungulia wazazi na Upasuaji Zahanati ya Gungu likiwa limegharimu kiasi cha Fedha Million mia mbili sabini (270,000,000/=), Uwekeaji wa Jiwe la Msingi Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa gharama ya Mradi ukiwa ni Million mia moja themanini na mbili (182,000,000/=), Uzinduzi wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na ofisi moja Shule ya Msingi Mwasenga vikiwa vimegharimu Million Sitini (60,000,000/=), Uzinduzi wa Maabara mbili kwa Shule ya Sekondari Mlole ukiwa umegharimu kiasi cha fedha Million arobaini na tisa laki tatu (49,300,000/=) na Utembeleaji wa chumba cha Tehama katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa
Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu wa 2021 ni Mbio maalum, umaalum wake pia unatokana na Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru kukimbizwa katika Wilaya za kiutawala tu za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania badala ya Halimashauri za Wilaya kama ilivyozoeleka, Na Wilaya ya Kigoma Mwenge wa Uhuru unatarajia kupokelewa kutoka Wilaya ya Uvinza Septemba 27 na Kutembelea, kukagua na kuzindua miradi pendekezwa huku Septemba 28 ukikabidhiwa katika Wilaya ya Buhigwe
Ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka 2021, unahusu matumizi sahisi ya TEHAMA, chini ya Kauli mbiu isemayo: “TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu .Itumie kwa usahihi na Uwajibikaji”. Pamoja na Ujumbe huo, Mbio za Mwenge wa Uhuru zitaendelea kuwakumbusha na kuwahamasisha wananchi na Viongozi kote nchini, kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI, Ugonjwa wa Malaria, mapambano dhidi ya matumizi ya Dawa za Kulevya, Mapambano dhidi ya Rushwa na kuhamasisha Wananchi juu ya Lishe bora kwa afya imara.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa