Na Mwandishi Wetu
Manispaa ya Kigoma/Ujiji Asubuhi ya Leo Septemba 21, 2025 imepokea Mwenge wa Uhuru ukitokea Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba amekabidhiwa Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Buronge.
Mwenge wa uhuru Manispaa ya Kigoma/Ujiji utakimbizwa Km 74 ambapo utazindua, kukagua na kuweka jiwe la Msingi katika miradi saba (07) yenye thamani ya fedha za Kitanzania 48,914,627,659.80.
Kauli Mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka huu ni" JitokeZe kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na utulivu".
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa