Na Mwandishi Wetu
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Mhe. Ngenda Kilumbe Shabani ametoa Majiko sanifu 400 kwa Wanawake wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa lengo la kuwezesha jamii katika matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia na utunzaji wa Mazingira.
Kiongozi huyo ametoa majiko Leo March 06, 2024 kwa Wanawake Mama lishe na Walengwa wa TASAF ikiwa ni Wiki ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Akikabidhi majiko hayo amewataka Wanawake kuendelea kuunga juhudi Serikali ya Awamu ya Sita na Maendeleo ya yanayotekelezwa katika Manispaa kwa mapato ya ndani na fedha kutoka Serikali Kuu.
Amesema Serikali imeendelea kuboresha utoaji huduma na miundombinu katika Hospitali ya Rufaa ya Maweni, Ujenzi na kuanza kutoa huduma katika Hospitali ya Manispaa iliyopo Kata ya Kagera, Ujenzi wa Shule, Zahanati, vituo vya afya na upatikanaji wa huduma ya maji katika Kata mbalimbali.
Amewataka kuendelea kutumia majiko bainifu ili kupunguza uchafuzi wa Mazingira na kuwa chachu kwa wengine katika kutumia nishati safi ya kupikia na kuzingatia suala la malezi ya familia na kupinga vitendo vya Ukatili kwa Wanawake na Watoto.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba amepongeza Mbunge wa Kigoma Mjini kwa jitihada za miradi ya maendeleo huku akiahidi kuendelea kusimamia ili iwanufaishe Wananchi.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa