Na Mwandishi Wetu
Wananchi na wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Leo Desemba 7, 2022 wameshiriki mazoezi ya viungo vya mwili katika kuendelea kuadhimisha Wiki ya Sherehe ya Miaka sitini na Moja (61) tangu Tanzania bara awali ikiitwa Tanganyika ilipojipatia Uhuru wake Desemba 9, 1961
Mazoezi hayo yamefanyika mapema Asubuhi yakianzia Stesheni ya Kigoma hadi Uwanja wa Mwanga Community Centre yakiongozwa na Kaimu Katibu tawala Wilaya ya Kigoma Ndugu. Maximillian Cyrillo huku zoezi la uchangiaji damu likifanyika katika uwanja huo
Kiongozi huyo amewapongeza Wananchi hao waliojitokeza kushiriki mazoezi hayo ikiwa ni njia ya uimarishaji na ukuzaji Kinga ya mwili na kuwapongeza namna walivyoshiriki kuchangia damu kwa lengo la kuokoa maisha ya watu
Tanzania bara awali ikiitwa Tanganyika kwa sasa inafahamika kwa jina la Tanzania kutokana na Muungano wake na Zanzibar mwaka 1964 na Kauli mbiu ya Mwaka huu ni " Miaka 61 ya Uhuru, Amani na Umoja ni nguzo ya Maendeleo yetu ".
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa