Na Mwandishi Wetu
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan imeendelea na utekelezaji wa uboreshaji wa huduma na Miundombinu ya afya katika maeneo mbalimbali Nchini Tanzania
Manispaa ya Kigoma/Ujiji ni miongoni mwa Halmashauri inayonufaika na uboreshaji wa miundombinu kwa lengo la kusogeza Huduma za afya Karibu na Wananchi
Fedha za Kitanzania Shilingi Million mia tatu ( Tsh 300,000,000/=) zilizopokelewa kutoka Serikali Kuu kwa lengo la ujenzi wa miundombinu katika Kituo cha afya cha Gungu
Miundombinu inayoendelea kujengwa ni jengo la kuwahudumia Wagonjwa wa Nje (OPD), Ujenzi wa Maabara, Ujenzi wa Jengo la kufulia Nguo za Wagonjwa na Ujenzi wa kichomea taka
Kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu hiyo kutawanufaisha Wakazi wa Kata ya Gungu na Kata jirani kwa kuhakikisha wanapata huduma bora na kuboreshwa kwa mazingira ya Watumishi katika utendaji kazi
Aidha Ujenzi wa Mradi huo umetoa ajira zaidi ya sabini (70) katika kazi mbalimbali zinazoendelea kutekelezwa kama vile fundi ujenzi, kuchanganya zege, ubebaji zege na tofali na wajasiriamali wanaopika vyakula jirani na eneo hilo
(Picha ni ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kigoma ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Bi. Ester Alexander Mahawe May 26, 2022 ilipotembelea Mradi huo)
#mamayupokazini #kaziiendelee #sensa2012 #jiandaekuhesabiwa
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa