Na Mwandishi Wetu
Vikundi vya Wajasiriamali Manispaa ya Kigoma/Ujiji vimeendelea kunufaika na mikopo isiyokuwa na riba ya 10% kutoka katika mapato ya ndani kwa vikundi vya wanawake, Vijana, na Watu wenye ulemavu huku wakiaswa kutumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa
Aliyasema hayo Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Ester Alexander Mahawe Jana Februari 15, 2022 katika ukumbi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji alipokuwa akikabidhi Mfano wa hundi wenye thamani ya Tsh 79,000,000/= kwa lengo la kuwanufaisha wanakikundi 200, Wanawake 183, vijana 10 na watu wenye ulemavu 07 kutoka katika jumla ya vikundi 12 vya wanawake, vijana na Watu wenye ulemavu
Alisema lengo la kugawa mikopo hiyo ni kwa ajili ya kuinua vikundi hivyo ili kujitegemea katika miradi yake na kuwa na uwezo wa kujiendesha na kuwa na uwezo mkubwa hata kukopa katika taasisi za fedha
Awali akiwasilisha taarifa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndugu. Athumani Msabila alisema Mkopo huo uliotolewa ni awamu ya pili kwa mwaka wa fedha 2021/2022, mkopo wa kwanza iliotolewa ilikuwa kiasi cha fedha Tsh 105, 500, 000/= ambapo ulinufaisha wanakikundi 300, Kati ya Wanawake 265, vijana 21 na watu wenye ulemavu 14 na Mkopo awamu ya tatu ukitarajiwa kutolewa Mwishoni mwa mwezi march 2022
Naibu Meya wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Mgeni Kakorwa alivitaka vikundi hivyo kutumia mikopo hiyo kwa miradi iliyokusudiwa na kurejesha fedha hizo kwa wakati ili kuendelea kukopa na kunufaisha vikundi vingine
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kigoma Alhaji Yassin Mtalikwa aliipongeza Manispaa ya Kigoma/Ujiji namna inavyotekeleza ilani ya Chama hicho kwa utoaji wa mikopo huku akisema Chama hicho kinaridhishwa na utendaji kazi wa Manispaa hiyo
Mmoja wa wanufaika wa miradi hiyo kutoka kikundi cha Wanawake Maendeleo Bi. Aisha alisema wapo tayari kutumia mikopo hiyo isiyokuwa riba katika miradi iliyotekelezwa huku akipongeza elimu inayotolewa kabla ya kutolewa kwa mikopo hiyo
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa