Mwandishi wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Ester Alexander Mahawe leo June 23, amefika katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji na kuongea na Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Watumishi wote huku akiwataka kufanya kazi kwa ushirikiano katika kuwatumikia Wananchi
Akizungumza na Watumishi hao Mkuu huyo wa Wilaya amewataka Watumishi wote kufanya kazi kwa ushirikiano na kuwahudumia wananchi na makundi mbalimbali pasipo kuwa na malalamiko na kufanya kazi kwa weledi
Akizungumzia usimamimizi wa miradi inayotekelezwa amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo wenye kutekeleza miradi kusimamia kwa weledi kwa kuzingatia ubora na viwango pasipo kutanguliza masilahi yao binafsi na kuacha miradi ikiwa na manufaa kwa Wananchi
“Mimi ni Mhandisi asiye kuwa na cheti nina uzoefu wa zaidi ya miaka ishirini na moja (21) katika kusimamia na kufuatilia miradi mbalimbali hivyo nawataka wakuu wa Idara na vitengo kuwa waaminifu na kusimamia viwango na ubora wa miundombinu” amesema Mkuu wa Wilaya huyo
Akizungumzia juu ya wahamiaji haramu amesema wilaya ya Kigoma imepakana na Nchi jirani ambazo wananchi wake huingia sana nchini Tanzania kupitia Ziwa Tanganyika na njia nyingine zisizokubarika huku akiahidi kudhibiti mianya hiyo kwa kusimamia vikao vya kamati ya ulinzi na usalama kufanyika kwa wakati kwa ngazi zote na wananchi kuishi kwa Uhuru na Amani
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Frednand Filimbi akimkaribisha Mkuu wa wilaya amempongeza kwa kuchaguliwa katika nafasi hiyo huku akisema Ofisi ya Mkurugenzi ikishirikiana na Wakuu wa Idara na Vitengo wako tayari katika kutoa ushirikiano katika utendaji kazi na kusimamia miradi katika ubora na viwango vinavyokubalika
Mkuu huyo wa wilaya ni miongoni mwa walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan June 19, 2021 ambapo June 21 aliapishwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma na Mkuu huyo wa Wilaya ameanza kufanya ziara yake kwa kuzungumza na Watumishi wa Ofisi mbalimbali na makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutembelea miradi
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa