Na Mwandishi Wetu
Manispaa ya Kigoma/Ujiji imeanza kutekeleza miradi ya uhifadhi wa mazingira na kuondoa kero kwa Wananchi katika Kata zote kumi na tisa (19) na mitaa sitini na nane (68) kupitia Mradi wa Tasaf
Miradi hiyo inatekelezwa huku ikitoa ajira kwa Wanufaika wa Tasaf wenye uwezo wa kufanya kazi kwa hiari kwa lengo la kuongeza ujuzi wa kufanya kazi, kuongeza kipato na uhifadhi wa Mazingira
Akizungumza katika ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi hiyo Mratibu wa Tasaf Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Izack Vyabandi amesema miradi sitini na tano (65) ndio inayotekelezwa na iliibuliwa kupitia mikutano ya Wananchi Mwaka jana 2022
Amesema miradi hamsini na tano (55) ni ya ukarabati wa barabara, miradi mitano (05) ni udhibiti wa korongo, miradi minne (04) ni ya upandaji wa Michikichi ya kisasa, na Mradi mmoja (01) ni uundaji wa dampo lisilo rasmi
Kipindi cha Pili cha TASAF Awamu ya Tatu ni cha miaka minne kuanzia 2020 – 2023, kiķiwa na Madhumuni ya kuongeza fursa za kujiongezea kipato na kuboresha huduma za kiuchumi na kijamii kwa kaya za walengwa
Kipindi cha Pili kinalenga kutengeneza njia mbadala na endelevu za ajira na kushiriki katika kazi za jamii na kupata kipato cha ziada kwa matumizi ya kaya na mahitaji mengine ya msingi na wakati huo wakiboresha miundombinu katika jamii na kupata ujuzi na stadi za maisha.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa