Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba amesema Halmashauri hiyo imetenga kiasi cha Million Mia moja tisini (Tsh 190,000,000/=) kwa ajili ya kujenga miundombinu (mifereji) ya kukusanya maji ya mvua katika Soko la Masanga.
Ameyasema hayo Leo Desemba 04, 2025 alipokuwa katika kipindi cha #Sikumpya kinachorushwa na Main FM iliyopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Amesema ujenzi wa mifereji ya kukusanya maji ya mvua unatarajia kuanza kabla ya mwezi January, 2026 kwa lengo la kuondoa kero ambayo imekuwa ikiwasumbua wafanyabiashara wa soko hilo.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa