Na Mwandishi Wetu
Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji imesaini mkataba wa ujenzi wa jengo la Utawala na Kampuni ya ujenzi ya Gopa Contractors Tanzania Limited kwa gharama ya fedha za Kitanzania zaidi ya Billion mbili (Tsh 2,486,056,280/=).
Mkataba huo umesainiwa kati ya uongozi wa kampuni ya ujenzi na Viongozi wa Halmashauri Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Mhe. Baraka Naibuha Lupoli na Mkurugenzi wa Manispaa Ndugu. Kisena Mabuba utiaji saini huo ukishuhudiwa na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Mhe. Kilumbe Shabani Ngenda.
Mradi huu unatekelezwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu ambapo hadi sasa Halmashauri imeshapokea kiasi cha fedha za Kitanzania Billion moja (Tsh Billion 1/=) na Ujenzi utafanyika kwa mda wa miaka mitatu (03) sawa na miezi 36 kuanzia tarehe ya Mkataba hadi Mwaka 2028 ambapo ujenzi utakuwa umekamilika.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa