Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba kwa kushirikiana na Taasisi ya Usilie tena, Na Mwalimu maarufu katika ufundishaji Yusuph Hamis amegawa bima za Afya na viti mwendo kwa Wanafunzi wenye Mahitaji Maalumu.
Bima ishirini na moja (21) na viti mwendo viwili (02) vimegawiwa Leo July 30, 2024 katika viwanja vya Ofisi kuu ya Mkurugenzi huyo huku zaidi ya Wanafunzi Mia moja na moja (101) wakiendelea na zoezi la picha ili kukamilishiwa na kukabidhiwa bima za afya.
Akizungumza katika tukio hilo Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ameitaka jamii kutowaficha watoto wenye ulemavu na kuhakikisha walemavu wanapata elimu, Mafunzo ya stadi za maisha na elimu ya kujitambua.
Aidha amempongeza Mwalimu Yusuph Hamis kwa namna ambavyo amekuwa akipambania makundi ya Wanafunzi wenye mahitaji Maalumu kwa kushirikiana na Wadau wengine wa elimu.
Awali akiwasilisha taarifa Afisa elimu Maalumu Elimu Msingi Ndugu. Ezekiel Mpanda amesema Manispaa ya Kigoma/Ujiji ina Wanafunzi wenye mahitaji Maalumu mia Sita thelathini na moja (631) kwa Shule za Msingi.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa