Na mwandishi wetu
Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Kamishina wa Polisi Salum Rashidi Hamduni leo June 18, 2021 amepanda miche ya zao la Michikichi katika Shule ya Sekondari Kasingirima iliyopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji alipokuwa akihitimisha ziara ya siku tatu Mkoani Kigoma aliyoifanya kwa lengo la kuadhimisha wiki ya utumishi wa Umma
Mara baada ya kupanda miche hiyo Kamishina huyo ameipongeza Serikali kwa kuamua kuinua zao la michikichi huku akisema jambo hilo litaleta tija Nchini kwa kuwainua wakulima wa zao hilo kutokana na uzalishaji wa mafuta mengi ya mawese na kuwataka wakulima kupanda miche hiyo katika mashamba yao
Aidha kiongozi huyo amefanya mazungumzo na Klabu ya wanafunzi wapiga rushwa waliopo katika shule hiyo huku akiwataka wanafunzi hao kuwa mfano mzuri wa kupinga viashiria na utoaji rushwa kwa kutoa taarifa katika mamlaka husika kuanzia ngazi ya Wilaya hadi Mkoa
Akitoa taarifa ya uzalishaji wa miche ya kisasa ya Michikichi Kaimu Mkuu wa Idara ya kilimo, Ushirika na Umwagiliaji Ndugu. Haruna Mtandanyi amesema Serikali imeamua kuwekeza katika zao la Michikichi ya kisasa itakayokuwa na uwezo wa kuzalisha ili kuzalisha tani nne(4) hekta kwa mwaka kutoka tani moja (1) hekta kwa mwaka kwa michikichi iliyokuwepo
Ameendelea kusema lengo la Halmashauri ni kuzalisha miche million moja (1,000,000) na kuigawa kwa wakulima bure na hadi sasa miche elfu thelathini (30,000) imegawiwa kwa wakulima, kupanda kando ya barabara na kupanda kwa baadhi ya taasisi za Serikali huku akiongezea kuwa ifikapo mwezi oktoba wakulima watagawiwa miche zaidi ya laki moja (100,000) bure
Kaimu mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu.Frednand Filimbi amempongeza Kamishina Mkuu wa Takukuru Nchini kwa kuamua kupanda zao la Mchikichi katika shule ya Sekondari Kasingirima, huku akisema kupanda kwake huko kutaleta hamasa kwa wakulima, jamii na wakazi wa Manispaa hiyo kuendelea kuona umuhimu wa kulima zao hilo
Viongozi wengine walioshiriki upandaji wa miche ya kisasa ya michikichi ni Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kigoma Stephen Mafipa, na Naibu wa Takukuru Mkoa wa Kigoma Nestory Gatawa
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa