Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Mwantum Mgonja amewataka wakazi wa Manispaa hiyo wanaoishi katika Kata zinazotekeleza Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki Ardhi (Land Tenure Improvement Project) kuchangamkia fursa za upatikanaji wa hati miliki za ardhi zinazotolewa bure
Ameyasema hayo Leo Augusti 17, 2023 alipokuwa akihutubia Kamati za Urasimishaji ardhi Kata ya Kagera za Mtaa wa Kanswa, Kibwe na Mkese alipofanya ziara katika Kata hiyo kwa lengo la kufanya kikao na kamati hizo
Akihutubia Wajumbe wa Kamati hizo ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dr. Samia Suluhu Hassani kwa namna ambavyo imeleta fedha za utekelezaji wa mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki Ardhi kwa Wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji
Amezitaka Kamati za Urasimishaji ardhi katika Kata zote zinazotekeleza mradi kuendelea kuwaelimisha Wananchi ili kujitokeza kushiriki kurasimishiwa ardhi na upangaji mji ili kuwa na makazi Salama
Mjumbe wa Kamati ya Urasimishaji Ndugu. Yassin Hamsini amemhakikisha Mkurugenzi kuwa wataendelea kutoa elimu na kuhamasisha Wananchi kujitokeza katika upatikanaji wa hati miliki kutokana na kuongezeka kwa thamani ya ardhi na upatikanaji wa fursa zingine
Wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji katika Kata za Kibirizi, kasingirima, Kagera, Gungu, Businde, Rubuga, Majengo, Kitongoni na Kasimbu wanatarajia kunufaika na upataji wa hati miliki za ardhi zaidi ya elfu kumi (10,000) bure katika Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki Ardhi (Land Tenure Improvement Project) ikiwa ni mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia (WB)
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa