Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais Tamisemi Dr. Rashid Mfaume amefanya ziara ya Kukagua na Kutembelea Hospitali ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji huku akihimiza ukamilishaji wa jengo la Maabara na Wazazi kwa wakati.
Ziara hiyo ameifanya Leo March 12, 2024 ambapo ameutaka uongozi wa Halmashauri kuendelea kusimamia Ujenzi wa majengo ili Wananchi waendelee kunufaika na huduma kwa sababu Majengo hayo kuwa ya kimkakati katika sekta ya afya.
Awali akiwasilisha Taarifa ya Hospitali hiyo Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Dr. Hashim Mvogogo amesema Hospitali hiyo ilizinduliwa Februari 19, 2024 kwa lengo la kuanza kutoa huduma za Matibabu kwa Wagonjwa wa nje (OPD), Mapumziko ya mda mfupi kwa Wagonjwa waliozidiwa na vipimo vya maabara.
Amesema Manispaa ilipokea Kiasi cha fedha za Kitanzania Billion Moja na Million Mia tatu (Tsh 1, 300, 000, 000/=) kwa ajili ya Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje ambalo limekamilika na linatumika, Jengo la Maabara, Jengo la Wazazi (Maternity Complex), Jengo la mionzi, na Stoo ya dawa ambapo Ujenzi unaendelea.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa